ALI KIBA (@OfficialAliKiba) ndiye mshindi wa Tuzo ya MTV EMA (BEST AFRICAN ACT)

0

cw16wuixaaavz2m-jpg_large

MTV Europe Music Awards 2016 ilifanyika weekend iliyopita ambapo Mtanzania mwimbaji staa wa bongofleva Alikiba alikua akiwania tuzo ya BEST AFRICAN ACT ambayo ilitangazwa siku ya tukio mshindi ni Mnigeria Wizkid.

Pamoja na kwamba Wizkid alitangazwa mshindi, mtandaoni ilikua inaonyesha Alikiba ndio anaongoza kwa kupigiwa kura na hapo watu wakaanza kuuliza kwa nguvu imekuaje? hata hivyo kulionekana mabadiliko baadae kwa rekodi hizo kutoonekana mtandaoni baada ya muda kupita.

ali

Taarifa za uhakika kutoka kwenye Management ya Alikiba Exclusive kwa millardayo.com ni kwamba wametumiwa taarifa na MTV EMA kwamba kuna kosa lilitokea lakini wamerekebisha na kumfikishia taarifa Wizkid kwamba tuzo haikuwa yake hivyo itachukuliwa na kupewa Alikiba.

Inaonekana Wizkid amefikiwa na taarifa na tayari post yake ya ushindi wa tuzo hiyo ameifuta kwenye mtandao wake.


Twitter: @chokadj @djchokatv

Instagram: @djchokatv @chokadj @djchokamusic

Facebook Fans Page: https://www.facebook.com/djchokamusic

Download DJChokaMusic Android Application Click HERE

Comments

comments