#AmkaNaJetman: Msaada unahitajika kwa Producer/Msanii huyu aliyelala kitandani miaka 5 baada ya kupooza mgongo.

0

Kwa Jetman, muziki ndiye rafiki yake mkubwa ambaye hawezi kumkatia tamaa licha ya kuwa kitandani kwa takriban miaka mitano baada ya kupooza mgongo.

Jetman ni producer na msanii wa dancehall anayeishi Mwanza aliyewahi kufanya vizuri miaka ya nyuma na vibao mbalimbali. Na sasa anahitaji msaada kutoka kwa wadau ili aweze kurejea kwenye hali yake ya kawaida.

“Hili ni suala ambalo nahitaji msaada, nahitaji msaada kabisa sababu nina maumivu makali sana kwahiyo kukaa ndio maana nashindwa,” anasema. Kwa sasa anatengeneza muziki akiwa kitandani na amekuja na mradi wa riddim.

“Kwahiyo ninachokiomba kwenu ni msaada ile kuweza kufikisha haya ninayoweza au kama kuna mtu anaweza kunisaidia mimi nikatibiwa, naweza kupata huo msaada,” anasema. Jetman anasema ameungana na wasanii wengine wa dancehall katika kusaidia muziki anaoufanya akiwa kitandani.

Shilingi milioni 12 zinahitajika ili aende India kupata matibabu. Tunaweza kuungana naye kwa kutengeneza nyimbo kwa kutumia riddim yake na kutoa mchango wa fedha za matibabu.
Wewe unaweza kuchangia kupitia 0757 62 62 07. Jina ni GODFREY KUSOLWA.

SOURCE: http://www.bongo5.com


Twitter: @chokadj @djchokatv

Instagram: @djchokatv @chokadj @djchokamusic

Facebook Fans Page: https://www.facebook.com/djchokamusic

Download DJChokaMusic Android Application Click HERE

Comments

comments