BIOGRAPHY: Oludemilade Martin Alejo (YCEE) from Nigeria

0

4

Akifahamika zaidi kwa jina analotumia jukwaani ambalo ni YCEE, Oludemilade Martin Alejo kama ilivyoelezwa na Bella Naija ni msanii maarufu Nigeria. Alianza kazi yake ya muziki mwaka 2012 kama msanii chipukizi kabla ya kusaini mkataba  na Tinny Entertainment.

Hata hivyo baada ya kupata nafasi ya kusoma Biokemia katika chuo kikuu cha Lagos aliacha kujishughulisha na masuala ya muziki kwa muda wa miaka miwili mpaka 2015. Alirudi tena katika ulimwengu wa muziki na wimbo wake wa ‘Jagabani’ na ‘Condo’ akishirikiana na Patoranking ambao ulimpandisha chati zaidi na kuteuliwa kushindania tuzo za ‘Ushirikiano wa Mwaka ‘ na ‘ Video bora ya mwaka’ kwenye  ‘Nigeria Entertainment Awards’ huko New York.

5

YCEE alipata umaarufu kimataifa mara baada ya kuteuliwa kushiriki katika mchakato wa ‘Revelation of the Year’ katika tuzo za muziki za MTV Africa Music Awards 2015 , na kuteuliwa tena katika tuzo za ‘Best Artist in African Pop’ mwaka 2015 kwenye tuzo za ‘All Africa Music Awards’. Pia alifanikiwa kuibuka mshindi wa tuzo za ‘Rookie of the year’ kwenye  The Headies mwaka huu.

Kwa sasa YCEE yupo chini ya lebo ya Tinny Entertainment, ambapo  anaendelea kukuza muziki wake kibiashara  kupitia wimbo wake mpya ‘Sun mi’ ambao ni  remix ya ‘ Condo ‘ akishirikiana na Khuli Chana wa Afrika Kusini, KiD X , sambamba na  DJ Consequence aliyeshirikiana nae hivi karibuni  katika wimbo mwingine ‘ In Benz ‘


Twitter: @chokadj@djchokatv

Instagram: @djchokatv@chokadj@djchokamusic

Facebook Fans Page: https://www.facebook.com/djchokamusic

Download DJChokaMusic Android Application Click HERE

Comments

comments