Mr.Tz awakilisha Tanzania katika mashindano ya Mr & Ms ASA of Maryland na anaombea support yetu.

0

15894649_1233388933383554_883979564105137450_n

Kama wengi mnavyojua mimi ni mgombea katika shindano la Mr & Ms ASA, Maryland, litakalofanyika Jumamosi Januari 28, 2017 katika chuo kikuu cha Bowie State. Huku siku ya shindano lenyewe ikiwa inakaribia nina maelezo mapya.

Upigaji kura kwa njia ya mtandao umeanza Jumatatu, Januari 9 katika tovuti ya marylandasa.com

Tafadhali hakikisha unaniunga mkono pamoja na #TeamJumbe

Natumia shindano hili kama jukwaa la kutangaza nchi yangu ya asili Tanzania ?? na kufundisha watu sehemu ya utamaduni, mila na muziki wetu. Najulikana kama Mr. Tanzania kwa hiyo ni wajibu wangu kuwakilisha, nchi yangu, mizizi yangu. Siwezi kufanikisha hili bila msaada wako. Naweka moyo wangu katika muziki na kila ninachofanya si kwa ajili yangu tu au wazazi wangu, au familia yangu bali ni kwa watu wangu & na nyinyi ndio watu wangu mnaonipa motisha. Bila nyinyi na uungaji mkono wenu siwezi kwenda mbele. Sisi ni wamoja kwa hiyo lazima tuungane mkono na kuwa pamoja katika hali na mali. Shindano hili ni fursa kuonyesha watu kutoka mataifa mbali mbali ya Afrika na kwingineko Tanzania ni nini, tunahitaji kuonyesha uwepo wetu juu ya jukwaa na katika safu za ushangiliaji. Natumaini utaniunga mkono.

15894439_1233388943383553_6015495988636533941_n

Tafadhali kumbuka upigaji kura mtandaoni umeanza Jumatatu, Januari 9 katika marylandasa.com.

Baada ya Januari 14 tiketi zinaweza kupatikana mtandaoni kwa $15.

Muunge mkono Mr Tz #TeamJumbe ? ??….Asili Haipotei

– Mr. Tz aka SanTz


Twitter: @chokadj @djchokatv

Instagram: @djchokatv @chokadj @djchokamusic

Facebook Fans Page: https://www.facebook.com/djchokamusic

Download DJChokaMusic Android Application Click HERE

Comments

comments