Nay wa Mitego Kuja na Tamasha la Nguvu ya Kitaa kwa Wanyonge

0

MSANII wa Hip Hop, Emmanuel Elibariki Nay the True Boy, amekuja na kampeni mpya ya kuwasaidia watu wa hali ya chini ambayo inaitwa Nguvu ya Kitaa. Kampeni hiyo itaanza rasmi kesho siku ya kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Julius Nyerere, Oktoba 14, yenye dhamira ya kuwasaidia watu hao ambao wanasapoti kazi zake na za wasanii kwa ujumla. Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 13, Nay amesema katika kampeni hiyo ambayo watatembelea Hospitali ya Tandale, nia ni kuwalipa fadhila watu wa kipato cha chini ambao wanafutilia kazi hizo lakini bado wanaishi katika mazingira magumu.


Twitter: @chokadj @DJChokaUpDates

Instagram: @ChokaDJ @DJChokaUpDates  @djchokamusic

Facebook Fans Page: https://www.facebook.com/djchokamusic

Download DJChokaMusic Android Application Click HERE

Comments

comments