NIKKI MBISHI: Sitohusika na mtu yeyote atakayeendelea kuusambaza au kuucheza wimbo wa “I’M SORRY JK”

0

Baada ya salamu naomba niombe radhi kwa vyombo vyote vya habari kuwa sitoweza kuwapa ushirikiano wowote kuhusu wimbo wangu wa “I’M SORRY JK” uliositishwa na hii ni kwa usalama wao na wangu pia.
Napokea simu nyingi sana zikihitaji maelezo juu ya suala hilo ila kiukweli kwa watakao hitaji taarifa kamili wanaweza kufika ofisi za BASATA,naomba nisiwe msemaji tena juu ya jambo hili.

Tahadhari:
Kwa yeyote atakayeendelea kuusambaza au kuucheza popote pale mimi sitohusika naye maana technology iko huru popote Duniani na siwezi kuzuia watu wasiupate kwa kuwa ushasambaa,hivyo chukua tahadhari ili usijikute mikononi mwa sheria ???. #Asanteni sana,naomba msubiri ujio wangu mpya wa #SINGELI na aina nyingine za muziki kama #NAIJA #MCHIRIKU n.k.
MUZIKI NI AJIRA,MUZIKI NI KAZI YANGU.
#Mungu_Simama_Kweli_Idhihirike
Ni wako mtanzania mvumilivu:

Nikki Mbishi @2017

With no offence!


Twitter: @chokadj @djchokatv

Instagram: @djchokatv @chokadj @djchokamusic

Facebook Fans Page: https://www.facebook.com/djchokamusic

Download DJChokaMusic Android Application Click HERE

Comments

comments